MADRID: Hispania yapambana na mtiririko wa wakimbizi
16 Septemba 2006Matangazo
Maafisa nchini Hispania wamesema takriban Wa-Asia 200 wametua kwa boti kwenye Visiwa vya Kanary. Inaaminiwa kuwa wakimbizi hao waliogunduliwa ndani ya boti moja,wanatokea Pakistan,Sri Lanka na India.Wa-Asia hao wamewasili Hispania wakati ambapo nchi hiyo imeanza kuwarejesha nyumbani Wa-Senegal walioingia Visiwa vya Kanary kinyume na sheria. Maafisa wa Hispania wamesema watu hao huenda wakarejeshwa makwao.Maafisa hao wamesema, mtiririko wa kama watu 24,000 kutoka Afrika, mwaka huu peke yake kwenye Visiwa vya Kanary ni janga la kiutu.