MADRID: Hispania itapeleka Lebanon wanajeshi 1,100
8 Septemba 2006Matangazo
Bunge la Hispania limekubali kuchangia wanajeshi 1,100 katika vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa vitakayopelekwa Lebanon.Kwa hivyo, Hispania,baada ya Ufaransa na Italia,itachangia idadi kubwa ya wanajeshi.Kiasi ya nusu ya wanajeshi hao wa Hispania,hii leo wanatazamiwa kuondoka bandari ya Rota katika manowari nne kuelekea Lebanon.Umoja wa Mataifa unataka kuwa na jumla ya wanajeshi 15,000 nchini Lebanon.Vikosi hivyo vya amani vinatarajiwa kuwasaidia wanajeshi 15,000 wa Ki-Lebanon kulinda sehemu ya kusini ya Lebanon na pia kuhifadhi eneo la usalama kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah.