1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid. Genge la kuwauza wanawake lavunjwa.

24 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEY3

Polisi wa Hispania wamesema leo kuwa wamevunja genge la Wanigeria ambao wanafikiriwa kuwa wanatengeneza faida ya Euro milioni 4 kwa kuwalazimisha wanawake wa Kinigeria nchini humo kuingia katika biashara ya umalaya na kuuza madawa ya kulevywa.

Jumla ya watu 18 wamekamatwa katika mji mkuu Madrid pamoja na Vigo ulioko kaskazini magharibi, Fuerteventura katika visiwa vya Cannary na Palma de Mallorca katika visiwa vya Baleary.

Polisi wamesema kuwa wanawake ambao wanakataa masharti ya genge hilo wanapigwa na kubakwa, na familia zao zinatishiwa kuuwawa. wanawake hao wanalazimishwa kulipa Euro 45,000 ili kuweza kuachiwa huru kutoka katika genge hilo.

Wakati wa kukamatwa jumla ya hati za kusafiria 29 za Nigeria, nyingi zikiwa za wanawake hao zilikamatwa, pamoja na fedha na kilo 1.4 ya madawa ya kulevywa , ya Kokaine.