MADRID Gaidi afungwa miaka 27 jela
26 Septemba 2005Matangazo
Mahakama kuu ya nchini Uhispania leo imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 27 jela kwa Imad Eddin barakat Yarkas baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mashambulio yaliyofanywa na magaidi terehe 11 mwezi septemba mwaka wa 2oo1 nchini Marekani.
Bwana Barakat Yarkas anadaiwa kuwa kiongozi wa mtandao wa Alkaida tawi la uhispania
Kwa jumla watuhumiwa 24 walifikishwa mahakamani leo mjini Madrid kwa sababu ya madai ya kuwa wanachama wa mtandao wa Alkaida.
Watatu kati yao wanatuhumiwa kushiriki katika mashambulio hayo.
Hatahivyo bwana Yarkas hakupatikana na hatia ya mauaji.