MADRID : ETA yashindwa kuripuwa bomu
10 Septemba 2007Matangazo
Wanamgambo wa kundi la ETA wa jimbo la Basque nchini Uhispania wamejaribu lakini wameshindwa kuripuwa bomu kubwa lililotegwa kwenye gari katika mji wa kaskazini wa Logrone.
Gari hilo lilikuwa limetegwa mabomu ya zaidi ya kilo 100 hapo jana.Masaa machache kabla ETA iliapa kuendeleza mashambulizi ya mabomu dhidi ya taifa la Uhispania.Pia hapo jana polisi ilivunja maandamano ya kuunga mkono wafungwa wa ETA kwenye mji wa Basque wa San Sebastian.
Polisi iliwakamata kiongozi wa kundi moja la haki za binaadamu na watu wengine watano.