1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Ecuador yathibitisha vifo vya raia wake wawili katika shambulio la bomu la Madrid.

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCe9

Serikali ya Ecuador imethibitisha kufa raia wake wawili kwenye shambulio la bomu lilitokea siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Madrid.

Shambulio hilo la bomu lilitekelezwa na kundi la ETA linalowania kujitenga.

Maafisa wa uokoaji wamesema huenda watu hao wamezikwa kwenye kifusi katika eneo la maegesho ya magari la uwanja huo.

Kiasi watu ishirini na sita walijeruhiwa.

Kundi la ETA lilikiri kuhusika na shambulio hilo na hivyo kukatiza mwafaka wa amani uliokuwa ukitekelezwa nchini humo tangu mwezi Machi.

Maelfu ya watu waliandamana dhidi ya ETA mjini Madrid na miji mingine, baadhi yao wakiitaka serikali ya Waziri Mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero kuondoka madarakani.