1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID : Castro anaendelea kupata nafuu uzuri

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfw

Daktari mashuhuri wa upasuaji wa Uhispania ambaye ndio kwanza amerudi nchini Uhispania kutoka Cuba kumfanyia uchunguzi kiongozi wa Cuba Fidel Castro amesema kiongozi huyo amekuwa akipata nafuu uzuri kutokana na operesheni ya upasuaji wa utumbo aliofanyiwa na kwamba anaweza kurudi tena kuiongoza nchi yake.

Kufuatia kurudi kwake mjini Madrid Jose Luis Garcia Sobredo pia amesema kwamba Castro hana ugonjwa wa kansa kama vile tetesi zilivyodokeza kwenye vyombo vya habari nchini Cuba kadhalika nchi za nje.

Castro mwenye umri wa miaka 80 amekuwa haonekani hadharani tokea mwishoni mwa mwezi wa Julai na mdogo wake Raul amekasimu kwa muda madaraka ya kuiongoza nchi.

Hata hivyo Shirika la Ujasusi la Marekani CIA linaamini kwamba hali ya Castro sio nzuri na kwamba wakati wowote ule anaweza kuutema.