1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid. Bomu lalipuka karibu na uwanja wa michezo.

26 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF06

Bomu limelipuka katika eneo la kuegeshea magari la uwanja wa michezo katika mji mkuu wa Hispania , Madrid. Hakuna taarifa za majeruhi.

Tahadhari ilitolewa katika gazeti moja kwa kuwahusisha wapiganaji wa ETA katika jimbo la Basque kabla ya mlipuko huo. Uwanja huo ni sehemu muhimu ya juhudi za mji wa Madrid za kutaka kuwa mwenyeji wa mashindano ya Olympics mwaka 2012.