1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID. Afisa wa zamani wa Argentina ahukumiwa.

20 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLT

Mahakama kuu ya Uhispania mjini Madrid imemhukumu afisa wa jeshi la wanamaji la Argentina kifungo cha miaka 640 gerezani kwa uhalifu dhidi ya binadamu alioufanya kati ya mwaka 1976 na 1983, wakati Argentina ilipokuwa chini cha utawala wa kijeshi.

Adolfo Scilingo wa miaka 58 alipatikana na makosa ya kuhusika katika visa vya mauaji ya wapinzani kwa kuwatupa kutoka ndegeni. Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema wapinzani elfu 30 wa kisiasa walitekwa nyara na kuuwawa wakati wa vita hivyo nchini Argentina.