Madereva wawili wa Shirika la Msalaba Mwekundu wauwawa Sudan
3 Mei 2024Matangazo
Taarifa ya shirika hilo inaeleza kuwa timu ya wafanyakazi hao ilikuwa njiani ikirejea kutoka Layba kutathmini hali ya kibinadamu ya jamii zilizoathiriwa na vurugu za kutumia silaha katika eneo hilo wakati tukio hilo lilipotokea.
Mzozo kati ya jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wanaongozwa na aliyekuwa makamu wake Mohamed Hamdan Daglo umesambaratisha nchi hiyo katika mzozo uliodumu kwa zaidi ya mwaka.
Vita hivyo vimeua maelfu ya watu na kuwalazimu mamilioni ya wengine kuyakimbia makazi yao katika kile ambacho Umoja wa Mataifa umekiita "Mzozo mkubwa zaidi wa watu kuhama makwao duniani."