1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madereva wa treni wafuta migomo mipya Ujerumani

14 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CpAU

BERLIN

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni nchini Ujerumani kimeondowa uwezekano wa kufanya migomo mipya na kimesema kwamba kiko tayari kuendelea na mazumngumzo juu ya mishara na shirika la reli la taifa.

Mkuu wa chama cha wafanyaakazi madereva wa treni GDL Manfred Schell amesema amejadili ongezeko la mshahara la asilimia 11 na Waziri wa Uchukuzi wa Ujerumani Wolfgang Tiefensee ambaye amekuwa akiusuluhisha mzozo huo.Schell amesema mazunguzo hayo ya pande tatu juu ya makubaliano kamili ya mshahara pia yataendelea.

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni kimekuwa kikifanya migomo kadhaa ya treni za abiria na mizigo iiliosababisha madhara makubwa tokea mwezi wa Julai na kimesema wanachama wake 34,000 wamekuwa wakilipwa mishahara ya chini kulinganishwa na wenzao barani Ulaya.