Maderava wa treni Ujerumani kugoma kwa saa 20
15 Novemba 2023Chama cha Madereva wa treni wa Ujerumani GDL kitaanza mgomo wa saa 20 kuanzia leo jioni hadi kesho baada ya kushindwa kuafikiana kuhusu nyongeza ya mishahara.
Mwenyekiti wa chama hicho, Claus Weselsky, amesema madai ya wafanyakazi ni ya msingi na kuwataka madereva na wafanyakazi wengine wanaowakilishwa na chama hicho, kujiunga na mgomo.Mgomo wa usafiri wa treni wa saa 50 Ujerumani wafutwa
Wafanyakazi wa treni wamekuwa wakishinikiza kuongezwa mishahara ili kukabiliana na mfumuko mkubwa wa bei ambao umeongezeka tangu mwaka uliopita. Mgomo huo ni wa hivi karibuni katika sekta ya uchukuzi kwenye taifa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.
Shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn limekiri kuwa mgomo wa leo utakuwa na athari kubwa. Mapema mwaka huu, kulifanyika mfululizo wa migomo ya chama kingine katika sekta ya usafiri, cha EVG, na kutatiza huduma ya usafiri.