Maelfu ya madaktari wadogo nchini Uingereza wameanza mgomo wa siku tatu unaotishia kuvuruga huduma kwa wagonjwa, wakishinikiza kuongezewa malipo. Mgomo huo ndiyo wa karibuni zaidi unaohusisha wafanyakazi wa shirika la taifa la huduma za afya la Uingereza, NHS. Ahmed Rajab ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Uingereza, alizungumza na Amina Abubakar kuhusu hili.