Madaktari wa mkoa wa Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameandamana hii leo mjini Bukavu kuishinikiza serikali ya Congo iwaboreshee viwango vyao vya mishahara, wakisema wamechoka kufanya migomo ya kila mara bila kujibiwa. Sasa wanaitaka serikali itimize ahadi zake. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Mitima Delachance kutoka Bukavu.