1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADA KUU ZA WAHARIRI WA MAGAZETI YA UJERUMANI LEO NI:DAI LA FRIEDERICH MERZ KUFUTA HIFADHI YA KUTOWAFUKUZA WAFANYI KAZI MAKAZINI NA KITISHO CHA VIKWAZO CHA UMOJA WA ULAYA KWA SUDAN

Ramadhan Ali27 Julai 2004
https://p.dw.com/p/CHPu

Gazeti la FRAKFURTER RUNDSCHAU likilichambua pendekezo hilo laandika:

"Yabainika bawa la Friedrich Merz chamani, haliridhiki na mageuzi madogo madogo yanayofanywa.Kwahivyo, linadai futa kinga inayowahifadhi wafanyikazi wasitimuliwe makazini; futa mezani sawa ya malipo kati ya wanyonge na wanaojiweza katika bima ya afya,futa pia mfumo wa kuwapokonya matajiri ili kuwapa masikini katika mfumo wa kodi.Madai haya hayahusu kabisa na kuijenga upya dola hii ianyowatunza wanyonge na wasiojiweza kay inapangwa kuyatekeleza chama hiki kikikamata madaraka.

Kwa mara ya kwanza mwenyekiti wa chama Bibi Angela Merkel, anamudu kuamua.Kwa kipindi kirefu kijach, haitatosha lakini kutegemea udhaifu wa chama-tawala cha SPD ili kutuliza mambo chamani.Utafika wakati, mwenyekiti huyo itambidi kuweka nidhamu chamani."-Hilo lilikua Frankfurter Rundschau.

Ama gazeti la Mittelbayerische Zeitung linalochapishwa Regensburg laandika:

"Kwa njia hii au ile, miaka 2 kabla uchaguzi mkuu ujao, mtafaruku unazidi ndani ya chama cha CDU.Mtu aweza kuuleza kuwa mtafaruku huo ni kama mchezo wa kuigiza wa majira haya ya kiangazi wakati ambao kila matamshi yanayotolewa hutiwa chumvi mno na vyombo vya habari.Kusema hivyo lakini, ni nusu ukweli.Ukweli ni pia katika uchunguzi wa maoni chama cha upinzani cha CDU ambacho kinaongoza kwa mwanya mkubwa ,katika medani ya maamuzi muhimu ya kisiasa juu ya hatima ya nchi hii,hakijui kinaelekea mkondo gani."

Katika gazeti la mji wa Cottbus-LAUSITZER RUNDSCHAU tunasoma kwamba, mjadala wa sasa kuhusu kufuta kinga ya kuwahifadhi wafanyikazi kufukuzwa makazini, unamurika hali inayojikuta chama hiki kwa jumla.Ingawa muungano wa Upinzani wa vyama vya CDU/CSU unaoongoza katika uchunguzi wa maoni ya wananchi, kama serikali bora kuliko hii inayotawala sasa ,unatoa sura ya vurugu tupu.Kwa muda mrefu Muungano huu wa Upinzani ukitumia udhaifu wa vyama-tawala na kuamini haungehitaji kuwaambia wananchi ungetawala vipi - matokeo yake:hakuna sasa anaelewa muungano wa CDU/CSU una sera gani ,kwani kila mmoja chamani anapiga debe lake."-hilo lilikua LAUSITZER RUNDSCHAU.

Likitubadilishia mada, gazeti la mji wa Hannover: HANNOVERSCHE ALLGEMEINE ZEITUNG laandika kwamba, Umoja wa ulaya umeitishia wazi wazi Sudan kuiwekea vikwazo:Gazeti lasema,

"Bila shaka, dhamana ya kuhilikishwa wakaazi wa kiafrika na wanamgambo wa kiarabu inaangukia mabegani mwa serikali ya Sudan.Ikiwa safisha-safisha ya kikabila inayofanyika huko Dafur haitazuwiwa na serikali yenyewe,basi Jamii ya kimataifa itabidi kuchukua hatua. Kitisho hiki ni cha wazi wazi na chaanzia shinikizo la kibalozi na vikwazo vya kiuchumi ambavyo vitajumuisha mashirika ya mafuta ya petroli yanayochimba mafuta nchini humo, hadi maandalio ya kujiingiza kijeshi.

Mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya na mwenziwao wa Marekani,wameanza uzuri:Wana wakati mfupi kuuepuisha Umoja wa mataifa kujitwika jukumu la kunusuru balaa jengine kubwa lisitokee."

WÜRZBURGER TAGESPOST latumalizia kwa kuchambua hivi:

" Kuwahilikisha klidogo-kidogo,wakulima wa kiafrika milioni 1.2 na wanamgambo wa kiarabu pamoja na kuwatimua kutoka vijiji vyao, ni ukabila wa aina dhaifu kabisa.

Ikiwa Rais Omar Al Bashir anadai mbinyo wa kimataifa juu ya mzozo wa mkoa wa Dafur,kimsingi, ni kuhujumu uislamu, hii ni upumbavu Lakini, inadhihirisha dai lake haraka namna gani watawala wa kiislamu wa Khartoum wanavyoitumia dini wakijikuta wameelemewa na mbinyo.Jinsi serikali ya Khartoum ilivyowatendea wakulima wa kiafrika huko Dafur si utu kabisa."