Macron, Scholz na Duda wajadili kuisaidia Ukraine
13 Juni 2023Rais Duda ambae ni mmoja kati ya waunga mkono wa dhati wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Ukraine inangoja ishara isiyo na mashaka kuhusu matarajio yake ya uwanachama wa Jumuiya ya Kujihami-NATO. Amesema anamatarajio kuwa mkutano ujao wa NATO ambao utafanyika Julai, huko Lithuania utatoa mwangaza wa matumaini kwa Ukraine, hatua ambayo ipo katika matamanio ya taifa hilo kwa muda mrefu.
Aliongeza kwa kusema hayo ndio matarajio ya uongozi wa Ukraine na wanajeshi ambao wapo katika uwanja wa mapambano katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi. Ukraine inatarajia kupata muongozo wa uelekeo halisi wa kujiunga na jumuiya hiyo ya kujihami ya mataifa ya Magharibi. Hii ni baaada ya Rais Zelensky kutanga za ombi la kuharakishwa kwqa mchakato huo mwaka uliopita.
Uhakika wa mattarajio ya Ukraine kujiunga na NATO
Lakini katika mkutano huu ambao ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa NATO, Macron alikuwa mwenye kujizuia zaidi katika hilo ukilinganisha na Duda akisema mkutano ujao wa NATO utajikita kuiunga mkono Ukraine, na kuipa muongozo unaostahili. Hali kama hiyo ipo katika mataifa mengine wanachama wa jumuiya hiyo kama Marekani na Ujerumani ambato zinazingatia sharti moja la jumuiya hiyo kwamba fursa ya kujiunga kwake si ushiriki wa migogoro ya kimataifa.
Kwa hivyo hata katika mkutano huu wa sasa Kansela Scholz alijitenga na kuzungumza lolote kuhusu mchakato huo na badala yake anasema juhudi kubwa kwa sasa zinalenga kuisaidia Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi. Na kwamba endapo itahitajika wataendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu."Kwa Ukraine, tumekuwa tukizungumzia kuhusu uhakika usalama.Uhakika wa usalama ambao ni muhimu kwa amani,ambao kwa bahati mbaya uko mbali kufikiwa. Kwa jinsi tunavyotamani kuona Ukraine ikifanikiwa kwa haraka kutetea nchi yake, mamlaka na mipaka yake, ni wazi kuwa kwa sasa juhudi zetu kuu zimeelekezwa katika kuiunga mkono Ukraine katika mapambano yake ya ulinzi, kama tunavyofanya kwa kuwapa silaha nyingi, misaada mingi ya kifedha na ya kibinadamu," alisema Scholz.
Jitihada ya kuisadia silaha zaidi Ukraine
Akizungumzia hali ya makablkiano ya ndani nchini Ukraine Rais Macron amesema mashambulizi ya Ukraine dhidi ya Urusi ambayo yalianza katika siku chache zilizopita yataweza kudumu kwa miezi kadhaa ijayo. Amesema taifa lake lingalipenda kuona Ukraine inafanikiwa katika hatua hiyo kwa haraka ili iweze kusababisha awamu ya mazungumzo kwa muongozo mzuri.
Katika siku za hivi karibuni Ufaransa imeongeza juhudi za kuipa silaha Ukraine. Macron ameiita vita ya Urusi ni uchokozi wa Urusi na kushindwa kwa siasa za kikanda.
Soma zaidi:Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anapanga kuzungumza na rais wa Urusi Vladimir Putin
Mikutano ya pande tatu iliyohusisha Ujerumani, Ufaransa na Poland, inajulikana kama "Weimar Triangle", ilianza 1991 huko Weimar, Ujerumani. Msingi wake ulikuwa kuisogeza Poland na mataifa mengine ya Ulaya ya Mashariki karibu na Umoja wa Ulaya na NATO.
Chanzo: DPA