1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron kutoa majibu kuhusu maandamano ya vurugu

5 Julai 2023

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameahidi kutoa majibu ya kimsingi katika mkutano na zaidi ya mameya 300. Mkutano huo uliandaliwa kujadili machafuko yaliyoikumba nchi hiyo kwa karibu wiki nzima.

https://p.dw.com/p/4TQsO
Paris Emmanuel Macron
Rais Emmanuel Macron katika mkutano na Mameya wa UfaransaPicha: Ludovic Marin/AFP/AP/picture alliance

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameahidi kutoa majibu ya kimsingi katika mkutano na zaidi ya mameya 300. Mkutano huo uliandaliwa kujadili machafuko yaliyoikumba nchi hiyo kwa karibu wiki nzima. Maandamano yalizuka kote nchini baada ya tukio la karibuni la kijana mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi wa barabarani. Macron amekiri kuwa kiwango cha vurugu kimepungua kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, alikuwa makini kusema kuwa ghasia zimekwisha. Rais huyo ameapa kuweka sheria ya dharura ili kushughulikia ujenzi mpya wa miundo mbinu iliyoharibiwa katika ghasia za karibuni. Baadhi ya vyombo vya habari pia vilimnukuu Macron akisema kuwa anatafakari kupiga marufuku mitandao ya kijamii. Rais hiyo aliimaumu mitandao ya kijamii kwa kusaidia kuchochea vurugu hizo.