1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron kuchangia dola milioni 36 Kongo

4 Machi 2023

Ufaransa itachangia dola milioni 36 katika mpango mpya wa msaada wa kibinadamu wa Umoja wa Ulaya kwa ajili ya mgogoro wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4OFzo
DRK Emmanuel Macron und Felix Tshisekedi
Picha: Ludovic Marin/AFP

Hayo yamefahamishwa leo na Rais Emmanuel Macron aliye katika ziara rasmi mjini Kinshasa.

Umoja wa Ulaya umetaja leo kuwa utaandaa mkakati wa kupeleka msaada wa kiutu huko Goma, katika eneo lililokumbwa na vita mashariki mwa Kongo na kwamba utatoa euro milioni 47 ili kusaidia mahitaji ya haraka kama vile chakula, maji, makazi na huduma za afya.

Soma zaidi: Rais wa Ufaransa Macron kufanya ziara ya siku nne Afrika ya Kati

Rais Macron amesema pia kuwa pande zote zinazohusika katika mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimekubali 'kuunga mkono' hatua ya usitishaji mapigano.

Kinshasa inaituhumu Kigali kuwaunga mkono waasi wa M23, tuhuma zinazokanushwa na Rwanda. 

Ziara ya Macron ina lengo la kufufua uhusiano uliyovunjika na mataifa kadhaa ya Afrika.