JamiiUfaransa
Macron aitetea sheria ya pensheni, maandamano yapangwa
18 Aprili 2023Matangazo
Rais Macron amesema hayo katika hotuba aliyotoa kwa njia ya televisheni. Ameeleza kwamba ni lazima kupandisha umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64 ili kuepusha kusambaratika kwa mfuko wa malipo ya uzeeni.
Soma pia: Macron asaini sheria tata ya pensheni, maandamano ya ghasia yazuka
Hata hivyo rais huyo amekiri kuwa mageuzi hayo hayaungwi mkono na amesema anatambua kwamba wananchi wamekasirika. Wanaoyapinga mabadiliko hayo nchini Ufaransa wamesema hotuba ya rais Macron haikusaidia kupunguza mivutano na jumuiya za wafanyakazi zimeazimia kuendelea na maandamano ya kupinga mabaidliko hayo.
Wakati rais Macron akitoa hotuba waandamanaji waliendelea na harakati zao nchini Ufaransa kote.