1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko ya Serbia hayawezi kuvumiliwa

23 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DC7r

BERLIN:

Serikali ya Ujerumani imeshutumu vikali uvamizi wa balozi za nchi za Magharibi uliofanywa na waandamanaji siku ya Alkhamisi katika mji mkuu wa Serbia,Belgrade.Waandamanaji hao walisababisha uharibifu mkubwa katika balozi hizo na ubalozi wa Marekani ulitiwa moto.Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema,yale yaliyoshuhudiwa barabarani nchini Serbia ni matukio yasiyovumilika.Ni matumaini yake kuwa vitendo vya aina hiyo havitorejewa na kutakuwepo hali ya utulivu.Wakati huo huo msemaji wa serikali mjini Berlin,Thomas Steg amesema,iwapo vitendo vya aina hiyo vitarejewa,basi uhusiano wa Umoja wa Ulaya na Serbia utapaswa kufikiriwa upya.

Siku ya Ijumaa,Waserbia kwa maelfu waliandamana katika Kosovo na Montenegro. Waandamanaji wenye asili ya Kiserbia katika mji wa Mitrovica,kaskazini mwa Kosovo,waliwashambulia polisi wa Umoja wa Mataifa katika machafuko yaliyozuka tangu viongozi wa Kosovo wenye asili ya Kialbania kujitangazia uhuru kutoka Serbia.Viongozi wa Serbia wamelaani machafuko yaliyotokea katika baadhi ya balozi za kigeni mjini Belgrade na wamesema ni vitendo vya wakereketwa.