Mkutano wa mawaziri wa biashara wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) unamalizika leo jijini Nairobi, huku ukizuka mvutano mkali kutokana na wajumbe kadhaa kupinga masuala yanayowasilishwa. Sikiliza mahojiano na Maurice Omondi, mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa Kenya wanaouza bidhaa za ngozi ambaye pia anahudhuria mkutano huo.