1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswidi

Mabalozi wa Urusi, Ukraine na Iran kutoalikwa Tuzo za Nobel

2 Septemba 2023

Wakfu unaosimamia tuzo mashuhuri duniani za Nobel leo umetangaza kuufuta mpango wa awali wa kuwaalika mabalozi wa Urusi, Belarus na Iran kuhudhuria halfa ya utoaji tuzo za Nobel iliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4Vsoh
Wirtschaftsnobelpreis - Medaille
Nembo ya Wakfu wa Tuzo za Nobel Picha: dpa

Uamuzi huo wa kutowakaribisha wanadiplomasia hao kwenye halfa hiyo ya mnamo mwezi Disemba inayopangwa kufanyika mjini Stockholm, Sweden, umefikiwa baada ya ukosoaji mkubwa tangu wakfu wa Nobel ulipotangaza siku ya Alhamisi azma ya kuwatumia mwaliko wawakilishi hao wa mataifa matatu.

Wakfu huo ulisema hapo kabla kuwa ungewaalika mabalozi wa Urusi, Belarus na Iran kwa lengo la kuwajumuisha hata wale wasio waumini wa maadili ya Tuzo za Nobel.

Tangazo hilo lilizusha malalamiko na wawakilishi wa vyama kadhaa vya siasa nchini Sweden walisema watasusia sherehe hizo.

Ukraine imeukaribisha uamuzi wa kufutwa mwaliko huo ikisema ni "ushindi kwa ubinadamu"