Mabaki ya Silaha za Libya bado ni tishio katika ukanda huo.
21 Mei 2013Ripoti iliotolewa na Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon inasema kuwa biashara ya meno ya tembo inatishia usalama wa tembo hao hasa katika nchi za Cameroon,Chad, Gabon na Jamhuri ya Afrika ya kati.
Bank-Monn amesema kuwa biashara haram ya meno ya tembo inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa vikundi vyenye silaha katika ukanda huo,likiwemo jeshi la Joseph Kony la Lord's Resistance Army LRA.
Amesema katika hifadhi ya Minkebe kaskazini mashariki mwa Gabon, zaidi ya tembo11,000 waliuawa kati ya mwaka 2004 na 2013 huku nchini Chad tembo 86 waliuawa na wengine 33 waliokuwa na mimba katika muda wa wiki moja tu.Katika hifadhi ya taifa Bouba Ndjida nchini Cameroon,zaidi ya Tembo 300 waliuawa ndani ya kipindi cha miezi miwili ya mwaka uliopita.
''Hali ilivyosasa,imefikia mamlaka za kitaifa katika baadhi ya nchi kama Cameroon imeamua kutumia jeshi lake,sheria na kutumia mawakala ili kuwasaka wawindaji wa tembo'' amesema Bank-Moon
Kwa upande wao maofisa wa umoja wa mataiafa wametaja sabubu ya kuuawa kwa tembo hao kuwa ni kutokana na kuzidi kwa mahitaji ya biashara ya meno ya tembo barani Asia,ambayo inachangia kuwapa motisha wafanyabiashara wa meno ya tembo.
Jopo la wataalamu wa umoja wa mataifa ambalo lilikuwa linafuatilia wimbi la mageuzi nchini Libya ambayo yalipelekea kuuawa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo,Muammar Gaddafi wanasema mwezi uliopita,nchi za Afrika Kaskazini zilikuwa chanzo muhimu cha silaha katika ukanda huo.
Wataalamu hao wanasema kuwa silaha hizo zilitawanywa kutoka Libya kwa hara zaidi na kuwasha moto nchini Mali,Syria na kwengineko na kutumbukia mikononi mwa waasi ambao wamezihifadhi katika ukanda huo, kwa ajili ya kuzitumia katika mapigano.
Joseph Kony anatuhumiwa kutumia silaha za Libya
Ripoti ya Bank-Monn imegusia pia silaha za Libya kutumika na jishi la Joseph Kony la LRA ambaye anatafutwa na Mahakama ya kimataiafa ya uhalifu wa kivita ICC kwa makosa ya uhalifu wa kivita
Joseph Kony na makamanda wake wanashitakiwa kwa kuwatumia watoto wadogo kama wapiganaji katika jeshi lake ambapo jeshi hilo limekuwa likipigana na serikali ya Uganda kwa miongo miwili sasa, kabla ya kufurushwa kutoka ngome yao Kaskazini mwa nchi hiyo mwaka 2005.
Ripoti hiyo ya umoja wa mataifa inasema kuwa Jeshi la Kony tayari limeua watu laki moja katika Jamhuri ya Afrika ya Kati miaka 25 iliopita,jeshi ambalo linalaumiwa kwa kutumia kati ya watoto 60,000 na 100,000 vitani na kuwaacha bila makaazi watu milioni 2.5
Ripoti hiyo imegundua kuwa LRA linahusika na mauaji ya zaidi ya watu100,000 na kwamba watoto100,000 wanaonekana kutekwa na jeshi la Kony ili kutumika kama wanajeshi.
Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa LRA linalaumiwa kwa kufanya mashambulizi 212 katika kipindi cha mwaka 2012 na kupelekea kuuawa watu 45 na wengine 220 wametekwa,robo yao wakiwa watoto wadogo.Jeshi lake pia linatuhumiwa kufanya utmwa wa ngono na matake wake.
Kony,ambaye alikuwa mtoto wa kanisani alianza mashambulizi yake dhidi ya serikali ya Uganda mapema mwaka 1980,Kundi lake sasa linafanya mashambulizi kwa nchi kadhaa sasa Afrika.
Kony anaetafutwa na mahakama ya ICC anadaiwa kujificha katika mipaka kati ya Sudan na Sudan Kusini,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na jamhuri ya Afrika ya kati
Mwandishi:Hashimu Gulana/RTE/ AFPE
Mhariri: Moahammed Abdul-Rahman