Kenya inalenga kuboresha miundo mbinu ya maji, wakati uhaba wa raslimali hiyo ukiripotiwa kuyakumba mataifa ya pembe ya Afrika, ikiwemo Kenya yenyewe, na majirani zake Somalia na Ethiopia. Kwa mujibu wa shirika kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, ni asilimia 29 tu ya Wakenya wanapata maji safi, hali inayotajwa kuchochewa na mabadadiliko ya tabianchi. Wakio Mbogho alituarifu zaidi.