Maandamano yaendelea kuitikisa Ufaransa
1 Julai 2023Machafuko hayo yanayofanywa na waandamanaji wanaodai haki kwa maisha ya mvulana huyo aliyetambulishwa kwa jina la Nahel yamesababisha uharibifu usio mfano.
Majengo na vyombo vya usafiri vimechomwa moto na maduka mengi yameporwa katika vurugu zinaoneskana kuwa changamoto kubwa kwa utawala wa rais Emmanuel Macron, tangu maandamano ya Vizibao vya Manjano yaliyoanza mwaka 2018.
Vurumai hiyo iliingia siku ya nne hapo jana na kusambaa karibu nchi nzima ikiwemo kwenye miji ya Marseille, Lyon, Toulouse, Strasbourg na Lille pamoja na mji mkuu Paris ambako Nahel alipigwa risasi na kuuwawa siku ya Jumanne.
Kijana huyo mwenye asili ya Algeria na Morocco alisimamishwa na polisi kwa makosa ya usalama barabarani lakini alijaribu kuwatoroka ndipo afisa mmoja alifyetua risasi iliyomuua.