Maandamano ya Ubelgiji yageuka kuwa vurugu
24 Januari 2022Baadhi ya maandamano yaligeuka kuwa vurugu ambapo kiasi watu 70 walikamatwa wakati wa maandamano hayo. Watu hao walikamatwa baada ya kukutwa na vifaa hatari au vilivyopigwa marufuku na wengine walikamatwa kwa kufanya uharibifu wa mali kwa mujibu wa msemaji wa polisi.
Maafisa watatu wa polisi na waandamanaji 12 walipelekwa hospitali baada ya kujeruhiwa.
soma zaidi: Ulaya yaimarisha vizuizi vya kukabiliana na virusi vya corona
Waziri mkuu wa Ubelgiji De Croo aliyalaani kwa maneno makali maandamano hayo akisema kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake lakini jamii haiwezi kuruhusu vurugu. Waandamanaji walionekana wakipeperusha bendera za Ujerumani, Poland na Ufaransa miongoni mwa nyingine.
Aidha walibeba mabango yaliyokuwa na maandishi ya kupinga chanjo.