Taarifa kutoka nchini Sudan zinasema Waziri Mkuu aliyepinduliwa na jeshi mnamo siku ya Jumatatu Abdallah Hamdok amerudishwa nyumbani kwake na ulinzi mkali umewekwa. Kwa mujibu wa wasaidizi wake Hamdok yuko nyumbani kwake pamoja na mkewe. Lakini pia maafisa wa usalama wamewakamata wanaharakati watatu maarufu wanaopigania demokrasia nchini humo.