1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano mjini Accra kupinga hali ngumu ya uchumi

6 Julai 2021

Wafuasi wa upinzani nchini Ghana wameandamana katika mji mkuu Accra wakipinga namna Rais Nana kufo-Ado anavyoshughulikia uchumi na pia kutaka haki kuhusu waandamanaji wawili waliouawa kwa kupigwa risasi mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/3w7EO
Ghana Accra| ECOWAS zur Lage in Mali | Nana Akufo-Addo
Picha: Nipah Dennis/AFP/Getty Images

Wakiimba nyimbo na kubeba mabango yenye ujumbe kama 'Kila mtu anateseka,' 'ishughulikie nchi,' 'Waghana wanakufa' na 'Akufo-Addo zinduka,' maelfu ya waandamanaji walijitokeza kwa amani katika mitaa mbalimbali mjini humo.

Maandamano hayo ya leo yalikuwa ya kwanza kuongozwa na chama cha National Democratic Congress (NDC) tangu mwezi Machi, wakati mahakama ya juu ilitupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa Akufo-Addo aliyechaguliwa tena mwaka uliopita.

Serikali ya Ghana ambayo imelemewa na madeni yanayozidi kuongezka pamoja na uchumi wake kuathiriwa pakubwa na janga la COVID-19, imeanzisha kodi mpya, imeongeza bei ya mafuta za bidhaa na huduma nyinginezo muhimu.