1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAANDAMANO KUDAI KAZI:

11 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkA
BAGHDAD: Kwa mara nyingine tena hii leo wafanya maandamano kwa mamia wamedai kupewa kazi na watawala walioikalia Iraq.Kwa wakati huo huo walilalamika kuhusu matumizi ya nguvu ya wanajeshi wa Kingereza na polisi wa Kiiraqi siku ya jumamosi.Kwa mujibu wa madaktari,si chini ya watu 6 waliuawa na wengi wengine walijeruhiwa siku ya jumamosi,baada ya machafuko kuzuka wakati wa maandamano ya kudai ajira.Wakati huo mjini Amara kiasi ya kilomota 360 kusini-mashariki mwa mji mkuu Baghdad,askarijeshi wa Kingereza na polisi wa Kiiraqi walipambana na maelfu ya Wairaqi walioandamana kulalamika dhidi ya ukosefu wa ajira.Kwa wakati huo huo zikapatikana habari kuwa Saddam Hussein huenda akafikishwa mahakamani mapema mwezi Julai.Mwongozi wa kiraia wa kimarekani nchini Iraq,Paul Bremer lakini amesema dhamana hiyo kwanza yapaswa kutolewa kwa serikali ya Wairaqi ikiwa ina mahakama yenye uwezo wa kusikiliza kesi ya aina hiyo.Kwa upande mwingine Baraza Tawala la Waiiraqi,limetuhumu hatua iliyochukuliwa na Marekani hivi karibuni kumtangaza Saddam Hussein kama ni mfungwa wa vitani.Wajumbe wa Baraza hilo wana khofu kuwa hifadhi atakayopewa dikteta huyo wa zamani wa Iraq kuambatana na Katiba ya Geneva,huenda ikaathiri kesi hiyo nchini Iraq.Kwa maoni ya wajumbe hao,Saddam Hussein ni mhalifu na apaswa kutendewa vilivyo.Halmashauri ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu sasa inajaribu kupata idhini ya kuonana na Saddam Hussein alie kizuizini.