1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa Palestina kuizuru China juu ya mzozo Gaza

20 Novemba 2023

Maafisa wakuu wa sera za kigeni kutoka mamlaka ya Palestina na mataifa manne ya Kiislamu wanatarajiwa kufanya ziara nchini China leo na kesho Jumanne.

https://p.dw.com/p/4Z9oO
Ahmad Mohammad Bahar / Kamati ya sheria ya Palestina PLC
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya kutunga sheria ya Palestina Ahmad Mohammad BaharPicha: Ali Jadallah/AA/picture alliance

Maafisa wengine katika ujumbe huo utakaoelekea China wanatokea Saudi Arabia, Jordan, Misri na Indonesia pamoja na jumuiya ya ushirikiano wa Kiislamu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning amesema, katika ziara hiyo, China itafanya mazungumzo ya kina na ujumbe unaojumuisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu na Kiislamu ili kuhimiza usitishwaji wa mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas, kuwalinda raia na kulitafutia ufumbuzi suala zima la mzozo wa Palestina.

Mamlaka ya Palestina, ambayo inatambulika kimataifa, inadhibiti sehemu za Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu japo haina udhibiti wa Gaza, ambayo inatawaliwa na Hamas.

Hamas limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na Marekani, Umoja wa Ulaya, Ujerumani na mataifa mengine.