Maafisa wa Marekani watuliza hali ya mambo Deir al Zor
4 Septemba 2023Maafisa wa vyeo vya juu wa Marekani wameutembelea mkoa wa mashariki wa Syria wenye utajiri wa mafuta wa Deir al Zor siku ya Jumapili katika juhudi za kutuliza uasi wa makabila ya kiarabu dhidi ya utawala wa Wakurdi unaoliyumbisha eneo la kaskazini mashariki la Syria.
Ubalozi wa Marekani nchini Syria umesema naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya eneo la mashariki Elthan Goldrich na meja Jenerali Joel Vowell, kamanda wa muungano unaoongozwa na Marekani unaopambana na kundi linalojiita dola la kiislamu IS nchini Syria na Iraq, wamekutana na maafisa wa Kikuridi na viongozi wa kikabila kutoka Deir al Zor.
Viongozi hao wamekubaliana juu ya umuhimu wa kuyashughulikia malalamiko ya wakazi wa mji wa Deir al Zor, vitisho vya wageni kuingilia mambo ya ndani na haja ya kuepusha vifo zaidi vya raia na majeruhi.
(Reuters)