1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa FIFA wachunguzwa kuhusu ufisadi

28 Novemba 2014

Maafisa watano, wakiwemo wanachama watatu wa kamati kuu ya FIFA waliohudumu kwa muda mrefu, wanachunguzwa kwa tuhuma za ufisadi kuhusiana na maombi ya kuchaguliwa mwenyeji wa Kombe la Dunia 2018 na 2022

https://p.dw.com/p/1Dwef
Schweiz Fußball FIFA Logo in Zürich
Picha: S. Bozon/AFP/Getty Images

Wanachama wa sasa wa bodi ya FIFA wanaofanyiwa uchuguzi ni makamu wa rais wa FIFA Angel Maria Villar wa Uhispania, Michel D'Hooghe wa UIbelgiji na Worawi Makudi wa Thailand.

Wengine wanaoshukiwa kufanyiwa uchunguzi ni nguli wa Ujerumani Franz Beckenbauer na Harold Mayne-Nicholls wa Chile. Beckenbauer alikuwa mpiga kura wa FIFA wakati bodi ilipoichagua Urusi kuandaa Kombe la Dunia mwaka wa 2018 na Qatar kupata kibali cha mwaka wa 2022. Aliachishwa kazi kwa muda wakati wa Kombe la Dunia mwezi Juni kwa kukataa awali kusaidia katika uchunguzi aliokuwa akifanya Michael Garcia.

Niersbach kugombea uwanachama

Tukibakia na masuala ya FIFA ni kuwa Kiongozi wa shirikisho la kandanda Ujerumani – DFB Wolfgang Niersbach atagombea uwanachama wa kamati kuu ya Shirikisho la Kandanda Ulimwenguni – FIFA mwaka ujao, kuchukua nafasi ya mwanachama wa Ulaya anayeondoka Theo Zwanziger.

Niersbach, ambaye ameikosoa kabisa FIFA kuhusu namna ilivyoishughulikia ripoti ya ufisadi katika kutoa vibali vya kuandaa Kombe la Dunia mwaka wa 2018 nchini Urusi na 2022 nchini Qatar, anassema Ujerumani inapaswa kuwa na sauti yake katika shirikisho hilo la kutoa maamuzi katika mchezo wa kandanda.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Josephat Charo