1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 yakubali kuanza kujiondoa mashariki mwa DRC

13 Januari 2023

Juhudi za Rais wa zamani nchini Kenya Uhuru Kenyatta za kurejesha amani nchini Congo zinaonekana kuzaa matunda baada ya waasi wa M-23 kukubali kujiondoa katika eneo lenye machafuko huko kivu ya kaskazini.

https://p.dw.com/p/4M9va
Kongo I Treffen zwischen EACRF und  M23-Rebellen
Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Haya yanajiri baada ya Uhuru ambaye kwa sasa ana wadhfa kama Mwezeshaji wa Mchakato wa Amani wa Afrika Mashariki katika eneo la Mashariki mwa DRC, kufanya mkutano wa faragha na viongozi wakuu wa kisiasa na wa kijeshi wa kundi la waasi wa M-23 mjini Mombasa.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Jumuia ya Afrika Mashariki, viongozi wakundi la waasi wa M-23 wamekubali kujiondoa kwa utaratibu na kuzingatia kuvisitisha vita vikali ambayo vimekuwa vikiendelea kwa muda katika eneo la kivu ya kaskazini mwa DRC.

Inasemekana  kuwa kundi hilo la waasi pia lilikubali kuheshimu na kushirikiana na kikosi cha kulinda amani cha Kanda ya Afrika Mashariki wakati kinachukua maeneo yaliyoachwa na wapiganaji wa M-23.

DR Kongo Kenias ehem. Präsident Uhuru Kenyatta in Goma
Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye ni mjumbe maalumu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki -CongoPicha: Benjamin Kasembe/DW

"Walizingatia na kutoa shukrani kwamba mashauriano ya Nairobi IV kati ya Kongo yatafanyika katika miji muhimu ya mashariki mwa DRC na hivyo kuleta mchakato wa Nairobi karibu na jamii mbalimbali zilizoathirika," taarifa hiyo ilisema.

Kufikia sasa Uhuru Kenyatta amefanikisha mikutano mitatu ya mazungumzo ya amani mjini Nairobi kati ya waasi na serikali ya DRC huku mashauriano ya nne yakiwa yamepangwa kufanyika katikati ya mwezi wa Februari mwaka huu wa 2023.

Kundi la M-23 kwa upande wao wametoa shukrani kwa Uhuru kwa juhudi zake za kuendelea kutafuta usaidizi wa kimataifa na ushirikiano unaolenga kurejesha amani mashariki mwa DRC na kupunguza mateso ya wananchi wa huko.

DRC: Waasi wa M23 wachukua udhibiti wa kijiji cha Nyamilima

Wawakilishi wa kundi hilo aidha wamemtaka Uhuru Kenyatta kusaidia katika kuhakikisha kwamba haki za raia zinaheshimiwa na kwamba makundi yote yenye silaha ya ndani na nje ya Kivu Kaskazini yanasitisha mapigano au mashambulizi dhidi ya M-23 wanapoondoka katika eneo hilo lenye hali tete. 

Aghlabu Uhuru amejitolea kujihusisha kibinafsi, kwa ombi la M-23, katika kuzuia matamshi ya chuki na matumizi ya lugha za uchochezi ambazo zinaweza kutatiza mchakato huo wa amani unaoendelea. Jambo ambalo limepongezwa na baadhi ya wakenya

"Ni muhimu kwamba Rais anapomaliza awamu yake na ana ujuzi wa kuendeleza masala kama ya amani na usalama katika maeneo ya nchi zetu ni jambo la busara na sisi kama wakenya lazima tujivunie sana tuone kama marais wa nchi nyingine waiga mfano kama huo miaka ijayo pakitokea jambo rais alostaafu awe anaweza kuendeleza maswala mengine ya kitaifa na mataifa mengine” Maimuna Mwidau Mchanganuzi wa maswala ya kisiasa na kijinsia amesema.DR:Congo: Waasi wa M23 wakabidhi kambi ya kijeshi ya Rumangabo, mashariki ya Kongo

Mkutano huo aidha ulibainisha kuwa eneo hilo lenye machafuko la Kivu Kaskazini nchini Congo limanza kuwa na usalama katika kipindi cha wiki nne zilizopita kwani watu wengi waliokuwa wamefurushwa kutoka makwao kufuatia machafuko wameanza kurejea nyumbani.