LUXEMBOURG:Mkutano juu ya bajeti ya Umoja wa Ulaya
13 Juni 2005Matangazo
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka jumuiya ya Ulaya wamekutana huko Luxembourg kwa mazungumzo yanayolenga kutatua tofauti zao juu ya suala la bajeti ya jumuiya hiyo ya mwaka 2007 hadi 2013.
Mojawapo ya suala kuu linalobishaniwa ni kiasi cha fedha kinachorudishiwa Uingereza kila mwaka kutoka Bajeti ya jumuiya hiyo.
Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso amemtaka waziri mkuu wa uingereza bwana Tony Blair afutilie mbali utaratibu huo. Lakini hadi kufikia sasa Uingereza inaonekana kutoafikiana na wazo hilo.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jack Straw amewaambia wanahabari muda mfupi baada ya kuwasili Luxembourg kwamba nchini yake itatumia kura ya Veto kutetea utaratibu huo wa kupokea fedha kutoka bajeti ya Umoja huo.