LUXEMBOURG: Vikosi vya Umoja wa Ulaya kuhifadhi usalama mpakani Chad
16 Oktoba 2007Matangazo
Umoja wa Ulaya umeidhinisha kupeleka kikosi cha wanajeshi 4,000 nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati kulinda wakimbizi wa Darfur katika maeneo ya mipakani.Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana amesema,kikosi hicho ni sehemu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kitasaidia pia kuhifadhi misaada ya kiutu katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya,operesheni ya tume hiyo itadumu mwaka mmoja.Wakati huo huo,Umoja wa Ulaya umetoa mwito kwa nchi za kanda hiyo ya mgogoro kushirikiana kuleta utulivu na usalama katika maeneo ya mpakani.