LUXEMBOURG. Umoja wa Ulaya watupilia mbali azimio dhidi ya Sudan.
21 Aprili 2005Matangazo
Mataifa ya umoja wa Ulaya yamefutulia mbali azimio lililowasilishwa kwa kundi la kutetea haki za binadamu la umoja wa mataifa, linaloilaani serikali ya Sudan kwa kuhusika na machafuko na ukiukaji wa hakai za binadamu katika eneo la Darfur. Badala yake zimekubali kuliunga mkono azimio pamoja na mataifa ya Afrika na ushirikiano na Sudan.
Msemaji wa Luxembourg amesema azimio hilo litatoa nafasi kukomesha ukiukaji wa haki za binadamu huko Darfur. Zaidi ya watu elfu 300 wameuwawa na wengine milioni mbili kulazimika kuyahama makazi yao wakihofu mashambulio ya wanamgambo wa janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya Khartoum.