LUXEMBOURG: Serikali mpya ya Wapalestina kupewa msaada wa pesa
19 Juni 2007Matangazo
Umoja wa Ulaya umerejesha uhusiano wake na serikali ya Wapalestina na unatayarisha kupeleka msaada,moja kwa moja kwa Wapalestina.Hatua hiyo imechukuliwa,baada ya Rais Abbas wa Fatah kuivunja serikali iliyokuwa ikiongozwa na Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas na kuunda serikali mpya ya dharura.Waziri wa masuala ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema,Umoja wa Ulaya una uhusiano mzuri na waziri mkuu mpya wa Wapalestina,Salam Fayyad.Akaongezea kuwa Umoja wa Ulaya utatoa msaada kwa serikali mpya ya Wapalestina.Wakati huo huo waziri wa masuala ya nje wa Israel,Tzipi Livni alipozungumza mjini Luxembourg alisema,sasa upo uwezekano wa kupeleka pesa kwa serikali hiyo mpya.