1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG. Romania na Bulgaria zasaini mikataba ya kujiunga na umoja wa Ulaya.

25 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJQ

Romania na Bulgaria zimetia saini mikataba ya kujiunga na jumuiya ya Ulaya hii leo, kandoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya mjini Lexembourg. Hatua hii imefungua milango kwa mataifa hayo kujiunga na jumuiya hiyo mwaka wa 2007.

Katika mkutano huo, umoja wa Ulaya umesisitiza Croatia haina matumaini ya kuanza mazungumzo ya kujiunga na jumuiya hiyo mpaka ishirikiane kikamilifu na waongoza mashtaka wa kimataifa wanaochunguza kesi za uhalifu wa kivita.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uholanzi, Ben Bot, amesema serikali yake inaamini raia wa Uholanzi wataiunga mkono katiba mpya ya umoja wa Ulaya, licha ya kura ya maoni ya mwishoni mwa juma kuonyesha raia wanaipinga katiba hiyo.