1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG : Hakuna ufumbuzi juu ya sera ya wakimbizi

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsE

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi za Umoja wa Ulaya wameshindwa kufikia ufumbuzi juu ya namna ya kuisaidia Malta kukabiliana na ongezeko la wahamiaji wasio halali.

Katika mkutano mjini Luxembourg Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schäuble amesema umoja huo wa nchi wanachama 27 kwa jumla ulikuwa tayari kuwajibika kwa pamoja lakini hilo lilikuwa ni jambo pekee ambalo mawaziri hao waliweza kukubaliana nalo.

Mpango wa Malta wa kuwasambaza wahamiaji hao kwa mujibu wa ukubwa wa nchi za Umoja wa Ulaya haukungwa mkono sana.

Wanaopinga mpango huo wanahofu kwamba wimbi la wakimbizi litafumuka iwapo kutafikiwa makubaliano hayo.

Mkutano huu unafuatia kushutumiwa kwa Malta kwa kukataa kuwachukuwa watu 27 waliokuwa wakin’gan’gania kwenye nyavu za uvuvi kwa siku tatu.