Lusaka. Wakimbizi wa Angola wakwama.
4 Septemba 2005Matangazo
Zaidi ya wakimbizi 700 wa Angola wanaotaka kurejea nchini mwao wamekwama nchini Zambia baada ya uchelewesho ambao haukutolewa maelezo na viongozi wa nchi yao kuiruhusu ndege inayotumika kuwarejesha, afisa wa umoja wa mataifa amesema leo.
Shirila la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR litafanya mazungumzo na maafisa wa Angola kesho Jumatatu katika juhudi za kutatua mzozo huo, ambao umesababisha wakimbizi 724 kukwama kwa muda wa siku kadha.