LUSAKA : SADC yakabiliwa na suala gumu la Zimbabwe
16 Agosti 2007Matangazo
Viongozi wa Kusini mwa Afrika wanatafakari njia za kupunguza makali ya matatizo ya kisiasa na kiuchumi nchini Zimbabwe katika mkutano wao wa viongozi unaoanza leo hii ikiwa ni siku moja baada ya serikali ya Zimbabwe kutangaza kukataa mazungumzo na upinzani.
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ya nchi wanachama 14 imekuwa ikishutumiwa kwa kumregezea mno Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na katibu mtendaji wa jumuiya hiyo amesema kwamba jumuiya hiyo inafikria hatua mbali mbali za kuchukuwa.
Tomaz Salomao ameuambia mkutanao wa waandishi wa habari hapo jana usiku kwamba mkutano huo wa siku mbili katika mji mkuu wa Zambia Lusaka kuwa hatua hizo zinajumisha msimamo mkali,diplomasia ya kimya kimya au njia nyengine tafauti