Lukashenko adokeza kupelekwa silaha za nyuklia kutoka Urusi
26 Mei 2023Udhibiti wa silaha hizo bado utabakia kwa Moscow.
"Ilikuwa ni juu ya Rais Vladimir Putin kunijulisha kuwa ametia saini amri juu ya hatua yetu ya kupeleka silaha za nyuklia Belarus. Tulikuwa tunazungumza juu ya hati maalum. Ndio, uamuzi ulichukuliwa ili kuendeleza kile kilichozungumzwa tu. Tulilazimika kuandaa maeneo ya kuhifadhi na mambo mengine huku Belarus. Tulifanya haya yote. Ndio maana vichwa vya nyuklia vilianza kuhamishwa," alisema Lukashenko.
Ukraine: Urusi inaishikilia Belarus kama mateka wa nyuklia
Rais wa Urusi Vladimir Putin mapema mwaka huu alitangaza kupelekwa kwa makombora ya masafa mafupi nchini Belarus, katika hatua inayochukuliwa kama onyo kwa mataifa ya Magharibi yanayoongeza usaidizi wa kijeshi nchini Ukraine.
Mpinzani wa Lukashenko, Sviatlana Tsikhanouskaya amelaani hatua hiyo na kuyaomba mataifa washirika kuchukua hatua za kuizuia.