Abinader aongoza matokeo ya uchaguzi wa rais wa Dominika
20 Mei 2024Rais aliyeko madarakani wa Jamhuri ya Dominika Luis Abinader ambaye ni mpambanaji mkubwa wa ufisadi, anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais kwa tofauti kubwa. Abinader anaongoza kwa asilimia 59 baada ya asilimia 38 ya kura kuhesabiwa, akifuatiwa na rais wa mara tatu Leonel Fernandez mwenye asilimia 26.
Abinader mwenye umri wa miaka 56 yuko kwenye mkondo wa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura na hivyo kuepusha duru ya pili ya uchaguzi. Msimamo wake mkali kuhusu Haiti na vita dhidi ya ufisadi vimemsaidia kupata uungwaji mkono zaidi kuliko wapinzani wake wakuu wawili. Jamhuri ya Dominica ´yakaza uzi´ mvutano wake na Haiti
Wapiga kura wapatao milioni 8 walishiriki katika kumchagua rais anayetazamiwa kuongoza juhudi za kutanzua mzozo wa jirani yake Haiti na vilevile kupambana na ufisadi katika taifa hiilo la Karibiani.