1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luanda. Shirika la afya duniani WHO latoa onyo kwa wasafiri kwenda Angola.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNE

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa kwa mara ya kwanza tahadhari ya kutosafiri kwenda Angola, ambako ugonjwa hatari wa Marburg umekwisha ua watu 210. Shirika hilo la afya limesema kuwa wasafiri wanatakiwa kuepuka kukaribiana na wagonjwa na kwamba watu wenye matatizo ya kiafya ambao huenda watahitaji huduma ya hospitali waache kwenda katika nchi hiyo. Msemaji wa shirika hilo pia amesema nchi zinaweza kuwachunguza watu wanaorejea kutoka Angola. Virusi vya ugonjwa wa marburg vinaambukizwa kupitia majimaji ya mwilini ikiwa ni pamoja na mate na damu. Ugonjwa huo umelikumba zaidi eneo la jimbo la kaskazini la Uige.