1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUANDA : Homa ya Marburg yauwa 230 Angola

16 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMX

Nchini Angola idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa gonjwa la virusi vya Marburg imeongezeka na kufikia watu 230.

Idadi hiyo inafanya kuwa mlipuko mkubwa kabisa wa gonjwa hilo kuwahi kushuhudiwa ambao mara ya kwanza uligunduliwa hapo mwaka 1967 wakati wafanyakazi wa maabara katika mji wa Ujerumani wa Marburg walipoambukizwa na kima kutoka Uganda.

Kitovu cha mlipuko huo ni mji wa Uige ulioko sehemu ya mbali kaskazini mwa Angola.

Virusi vya Marburg vinaweza kuuwa mtu mwenye afya katika kipindi cha juma moja kutokana na kuharisha na kutapika kunakofuatiwa na kuvuja damu ndani ya mwili na hadi sasa hakuna dawa inayojulikana inayoweza kuutibu ugonjwa huo.