Louise Arbour kuwa Mjumbe wa Haki za Binadamu wa UM
21 Februari 2004Matangazo
NEW YORK: Mwanasheria wa Kikanada Bibi Louise Arbour ameteuliwa kuwa Mjumbe Maalumu Mpya wa Haki za Binadamu wa UM. Mjini New York, Katibu Mkuu Kofi Annan alitangaza kuteuliwa rasmi kwa Bibi Arbour mwenye miaka 57. Bibi Arbour aliyekuwa Mtoa Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya UM ya Kuhukumu Wahalifu wa Kivita mjini The Hague, Uholanzi, atakuwa mfuasi wa Sergio Vieira de Mello, aliyeuawa hapo mwaka jana makao makuu ya UM mjini Baghdad yaliposhambuliwa kwa bomu. Mashirika ya Kimataifa ya Haki za Binadamu yamekaribisha kuteuliwa kwa Bibi Arbour ambaye kuteuliwa kwake kutabidi kuidhinishwa na Hadhara Kuu ya UM.