1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Waziri mkuu Tony Blair asema wanajeshi wataendelea kubakia Iraq

28 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEX0

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ameendelea kushikilia msimamo wake wa kukataa kuyaondosha katika siku za karibuni majeshi yake nchini Iraq.

Akihutubia mkutano wa kila mwaka wa chama chake cha Labour waziri mkuu Blair alieza kwamba njia ya kuelekea katika kipindi cha tatu serikalini kwa chama chake ni kuendelea na mageuzi ya huduma za jamii.

Hata hivyo Tony Blair hakusema ni lini anaweza kung’atuka madarakani kama kiongozi wa chama cha Labour.