LONDON:Uingereza yalitaka baraza la usalama la umoja wa Matifa kujadili ya Zimbabwe
27 Juni 2005Matangazo
Uingereza imelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kujadili juu ya suala la kuvunjwa nyumba nchini Zimbabwe.
Uingereza imekitaja kitendo hicho cha serikali ya mugabe kuwa kinakwenda kinyume na haki za binadamu.
Hii leo serikali ya Zimbabwe imesema itaanzisha mpango mpya wa ujenzi wa nyumba baada ya kuzivunja nyumba za walala hoi zilizokuwa mijini.
Takriban watu laki tatu sasa hawana makazi nchini Zimbabwe.