LONDON:Shirika la Kutetea haki za binadamu lataka NATO iache kupeleka wafungwa Afghanistan
13 Novemba 2007Shirika la kutetea haki za binadamu duniani Amnesty International limetoa mwito kwa nchi za NATO zinazolinda amani nchini Afghanistan kuacha kupeleka wafungwa nchini humo.
Shirika hilo limesema katika ripoti yake kwamba wafungwa hao wanateswa wanapoingia katika mikono ya maafisa wa Afghanistan
Asasi hiyo ya kupigania haki za binadamu pia imesema , nchi za NATO zinafumbuia macho mateso kwa kuendelea kupeleka wafungwa katika jela za Afghanistan.
Amnesty International imekariri inachoita matendo ya mateso na kukiukwa haki za binadamu yanayofanywa na idara za usalama za Afghanistan.
Sheria ya kimataifa inapiga marufuku kupeleka wafungwa katika sehemu ama nchi ambapo mateso ama ukiukaji wa haki za binadamu wa aina yoyote unatuhumiwa kutendeka.