LONDON:Mbeki asema Mugabe atang´atuka kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani
3 Aprili 2007Matangazo
Rais Thabo Mbeki wa ASfrika Kusini amesema kuwa anaamini Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe atang’atuka kwa amani kabla ya uchaguzi mkuu ujayo wa urais nchini humo.
Rasi Mbeki ameanza kazi ya kusaidia kutafuta suluhisho la mzozo wa kisiasa na kiuchumi unaoikabili Zimbabwe baada ya kuteuliwa na wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC wiki iliyopita.
Wakati huo huo mgomo uliyoitishwa na vyama vya wafanyakazi nchini humo kumshikinikiza Rais Mugabe umeonekana kuupuzwa.
Mapema Serikali ilisema kuwa mgomo huo ni haramu na kusema yoyote atakeyeuunga mkono atachukuliwa hatua za kisheria.